KARIBUNI!
Karibu katika ukurasa wa Deutsch Tansanische Freundschaftsgesellschaft kwa kifupi DETAF, maana yake ni Chama cha urafiki kati ya wajerumani na watanzania wanaoishi Ujerumani na ni chama cha watu wanaopenda kustawisha urafiki na mawasiliano kati ya mataifa haya mawili.
Katika kurasa zifuatazo utakuta maelezo kuhusu chama chetu,washirika wetu na miradi iliyoko Tanzania na jinsi unavyoweza kuwaunga mkono. Kupitia DETAF vijana wanaotaka kujitoa kufanya mazoezi kwa vitendo wanatumwa kusaidia katika miradi hiyo na zaidi ya hapo tunatoa maelezo mengi ya kila aina kwa wanaopenda kujua zaidi kuhusu Tanzania.