|
Deutsch-Tansanische Freundschaftsgesellschaft e.V. |
Kuhusa chama |
![]() |
||||
![]() |
||||||
DETAF ni nani?Chama cha urafiki kati ya wajerumani na watanzania (DETAF)) ni chama kisicholeta faida ambacho kinalenga kuzidisha uelewano wa kimataifa. Kwa kipindi kifupi, historia inawaunganisha Watanzania na Wajerumani. Hiyo pia ni sababu moja ya kupenda kukuza urafiki kati ya mataifa yetu mawili na kurahisisha uhusiano wa kisayansi, kiakili, kitamaduni, kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Ujerumani. Chama cha DETAF kinafanya nini?Tunaandaa matukio ya kielimu Ujerumani na kutunza mawasiliano na watanzania na marafiki wa Tanzania na pia tunasimamia huduma ya habari za Ujerumani na Tanzania. Tunaunga mkono kazi za washarika wetu wa miradi Tanzania na tunatoa miradi na ubia kwa watakaopenda. Jambo muhimu jingine katika kazi yetu ni kutuma vijana kwenda kushiriki katika miradi Tanzania. Zaidi ya hapo tunashauri wanaotaka kupokea wageni wenzao kutoka Tanzania na pia wale wanaotaka kwenda Tanzania kwa muda.Chama chetuChama cha DETAF kiliundwa Novemba 1986 na raia wajerumani na watanzania.. Anayetaka kupata habari kamili kuhusu shughuli zilizofanyika miaka iliyopita anaweza kusoma tariri (chronik) zetu ama nyaraka (archive) zetu kwa lugha ya kiingereza.Wanachama wetuWanachama wa DETAF ni wajerumani wanaopenda kujua zaidi kuhusu Tanzania na watanzania wanaoishi na kufanya kazi au kusoma ujerumani. Wanachama wetu wengi waliwahi kufanya kazi Tanzania katika mashirika ya maendeleo, lakini pia tunawakaribisha wote wanaopenda kuwa na urafiki kati ya Ujerumani na Tanzania.ShukraniTunapenda kumshukuru Richard Madete ambaye kwa miaka mingi alikuwa webmaster wa chama chetu. Richard Madete alirudi Tanzania mwaka wa 2006 mwishoni. Yeye ndiye aliyetuwezesha kupata ukurasa wetu katika mtandao mwaka wa 1995 na kuushughulikia tangu hapo. Ingawa imekuwa lazima kuubadilisha ukurasa huo hatutasahau jinsi Richard Madete alivyojitolea kwa dhati kuitambulisha DETAF. Tunasema ASANTE SANA. |
||||||