KARIBUNI!


Karibu katika ukurasa wa Deutsch Tansanische Freundschaftsgesellschaft kwa kifupi DETAF, maana yake ni Chama cha urafikikati ya wajerumani na watanzania wanaoishi Ujerumani na ni chama cha watu wanaopenda kustawisha urafiki na mawasiliano katiya mataifa haya mawili.

Katika kurasa zifuatazo utakuta maelezo kuhusu chama chetu,washirika wetu na miradi iliyokoTanzania na jinsi unavyoweza kuwaunga mkono. Kupitia DETAF vijana wanaotaka kujitoa kufanya mazoezi kwa vitendo wanatumwa kusaidia katika miradi hiyo na zaidi ya hapo tunatoa maelezo mengi ya kila aina kwa wanaopenda kujua zaidi kuhusu Tanzania.


DETAF ni nani?

Chama cha urafiki kati ya wajerumani na watanzania (DETAF)) ni chama kisicholeta faida ambacho kinalenga kuzidisha uelewano wa kimataifa. Kwa kipindi kifupi, historia inawaunganisha Watanzania na Wajerumani. Hiyo pia ni sababu moja ya kupenda kukuza urafiki kati ya mataifa yetu mawili na kurahisisha uhusiano wa kisayansi, kiakili, kitamaduni, kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Ujerumani.

Chama cha DETAF kinafanya nini

Tunaandaa matukio ya kielimu Ujerumani na kutunza mawasiliano na watanzania na marafiki wa Tanzania na pia tunasimamia huduma ya habari za Ujerumani na Tanzania. Tunaunga mkono kazi za washarika wetu wa miradi Tanzania na tunatoa miradi na ubia kwa watakaopenda. Jambo muhimu jingine katika kazi yetu ni kutuma vijana kwenda kushiriki katika miradi Tanzania. Zaidi ya hapo tunashauri wanaotaka kupokea wageni wenzao kutoka Tanzania na pia wale wanaotaka kwenda Tanzania kwa muda.

Chama chetu

Chama cha DETAF kiliundwa Novemba 1986 na raia wajerumani na watanzania.. Anayetaka kupata habari kamili kuhusu shughuli zilizofanyika miaka iliyopita anaweza kusoma tariri (chronik) zetu ama nyaraka (archive) zetu kwa lugha ya kiingereza.

Wanachama wetu

Wanachama wa DETAF ni wajerumani wanaopenda kujua zaidi kuhusu Tanzania na watanzania wanaoishi na kufanya kazi au kusoma ujerumani. Wanachama wetu wengi waliwahi kufanya kazi Tanzania katika mashirika ya maendeleo, lakini pia tunawakaribisha wote wanaopenda kuwa na urafiki kati ya Ujerumani na Tanzania.
Anwani Ya Posta
DETAF e.V.
Riesweg 22
26316 Varel

Mambo ya benki

DETAF - Spendenkonto
Akaunti Ya Idadi: 100768011
Bensberger Volksbank e.G.
BLZ: 370 621 24
BIC: GENODED1BGL
IBAN: DE88 3706 2124 0100 7680 11